ABOUT US


HISTORIA YA SHIRIKA LA DICHE FOUNDATION (2019)

1.    SHIRIKA LA DICHE FOUNDATION LILIANZISHWA TAREHE 12/12/2019 KUPITIA MKUTANO WA KIKAO CHA     WAANZILISHI WA SHIRIKA CHINI YA MWENYEKITI WAKE ALUKO LUKOLELA (SIR ALUKO)

2.    SHIRIKA LA DICHE FOUNDATION (2019) LIMETOKANA NA  MAWAZO NA KUWIWA MIONGONI WA WAANZILISHI NA KUTOKANA NA MATATIZO YANAYO WAKABILI WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU,  WAMAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 5 LISHE PAMOJA NA MAZINGIRA

3.    WAANZILISHI WA SHIRIKA LA DICHE FOUNDATION (2019)
      i.        SIR ALUKO                        – MWENYEKITI
     ii.        NEEMA HEZRON                 – KATIBU
    iii.        BAHATI SAIDI                    – KATIBU MSAIDIZI
   iv.        SAIDI KASSIM                    – MHASIBU
    v.        KASIM KASIM                              – MJUMBE
   vi.        ABEID MEZA                      - MJUMBE
  vii.        JUMA MRUMBE                  - MJUMBE
 viii.        RECHO RWECHUNGURA      - MJUMBE

4.    DHIMA YA SHIRIKA
Kuhakikisha taarifa za walengwa wa Shirika zinapatikana kwa ajili ya matumizi ya Njia bora za kuwahudumia kwa kuzingatia mahitaji yao ya sasa na ya baadae kwa kuishirikisha Jamii kupitia mikutano  Midahalo, Washa, Kongamano, Makala katika majarida, magazeti, vipeperushi, Runinga na Redro za Kijamii (Community Radio)
5.   HUDUMA ZITOLEWAZO NA SHIRIKA LA DICHE FOUNDATION 2019
Kufanya sensa ya kuwatambua watu wenye mahitaji maalumu kwa kupitia mamlaka za Serikali za Mitaa, viongozi wa dini, viongozi wa kisiasa na viongozi wa kimila kwa kushirikisha Jamii yenyewe kwa kutembelea nyumba hadi nyumba la Eneo husika.
6.     kutoa Elimu kwa Jamii umuhimu wa Afya ya Mama Mjamzito na Watoto wenye umri  chini ya miaka 5 kwa kushirikisha Jamii.

7.     Kuwaungania watu mbalimbali, mashirika ya ndani na nje katika kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum na wamama wajawazito kuwasaidia kupata huduma za msingi kama vile; Afya, Elimu, Chakula, Makazi na Mavazi

8.    Kuhakikisha upatikanaji wa vitendea kazi na vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa watoto wenye mahitaji maalumu vinapatikana kwa kuishirikisha Jamii, watu binafsi, pamoja na mashirika mbalimbali kutegemea na aina ya ulemavu alionao mtoto.

9.    Kuhakikisha shirika linakuwa na kituo chake cha Redio na TV kitakachosaidia katika kuelimisha Jamii suala zima la umuhimu wa kuwahudumia watoto walemavu, wamama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka 5 pamoja na mazingira.
CHANZO CHA FEDHA
i.             Michango iliyotolewa na waanzilishi wenyewe kila mmoja ametoa Tshs. 200,000/=
ii.             Viingilio vya wanachama kila mmoja  anapaswa atoe Tshs. 50,000 kama kiingilio na Ada ya kila mwaka 120,000/=
iii.            Misaada kutoka kwa wahisani na Serikali, Mashirika na Watu Binafsi
iv.           Ununuaji wa hisa kutoka makampuni na mashirika mbalimbali

v.             Harambee



0 comments:

Post a Comment

recent posts