SERVICES


Kufanya sensa ya kuwatambua watu wenye mahitaji maalumu kwa kupitia mamlaka za Serikali za Mitaa, viongozi wa dini, viongozi wa kisiasa na viongozi wa kimila kwa kushirikisha Jamii yenyewe kwa kutembelea nyumba hadi nyumba la Eneo husika.
1.     kutoa Elimu kwa Jamii umuhimu wa Afya ya Mama Mjamzito na Watoto wenye umri  chini ya miaka 5 kwa kushirikisha Jamii.

2.     Kuwaunganisha watu mbalimbali, mashirika ya ndani na nje katika kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum na wamama wajawazito kuwasaidia kupata huduma za msingi kama vile; Afya, Elimu, Chakula, Makazi na Mavazi

3.    Kuhakikisha upatikanaji wa vitendea kazi na vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa watoto wenye mahitaji maalumu vinapatikana kwa kuishirikisha Jamii, watu binafsi, pamoja na mashirika mbalimbali kutegemea na aina ya ulemavu alionao mtoto.


4.    Kuhakikisha shirika linakuwa na kituo chake cha Redio na TV kitakachosaidia katika kuelimisha Jamii suala zima la umuhimu wa kuwahudumia watoto walemavu, wamama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka 5 pamoja na mazingira.

0 comments:

Post a Comment

recent posts